Katika hospitali moja maarufu hapa jijini.Daktari mmoja anaehudumia wodi ya vichaa alitaka kuwajaribu wagonjwa wake wa akili kwa kuwafanyia jaribio moja ambalo kama mgonjwa angelifaulu basi daktari angemruhusu kwenda nyumbani. Daktari alichora mlango tofauti na ule wa wodini kwa kutumia chaki,na akaruhusu kila mgonjwa atoke wodini,lakini alimwona mgonjwa mmoja yeye akiwa pembeni anawacheka wenzake wanavyogombania kutoka nje katika ule mlango uliochorwa. Daktari akamuuliza: Na wewe mbona unawacheka wenzako? Daktari mi nawashangaa wenzangu wanagombaani kutoka nje wakati mi ufunguo wa huo mlango ninao