Kuna Mume na Mke ,walienda
shambani na kuukuta uyoga
mzuri ila hawakuwa na
uhakika kama uyoga ule
haukuwa na sumu.
Walikubaliana kumpa mbwa ilikujidhibitishia. Walipofika
nyumbani walipika na kisha
kumpa mbwa. Siku hiyo
mbwa hakupata madhara
yoyote. Siku iliyofuata baada
ya akuamka cha kwanza ni kumtazama mbwa. Mbwa
alikuwa salama salimin!
Wakajiridhisha kuwa uyoga
hauna sumu. Wakaenda
shamba na kuchuma uyoga
wa kutosha. Waliporudi mke aliuandaa na familia yote
ikala. Ilipofika saa 12 jioni
mtoto aliingia kasi na
kusema: "Baba mbwa
amekufa,anatoa damu
mdomoni" hapo wakajua kuwa kumbe uyoga
unaua,taratibu hivyo na wao
kesho watakufa.NO WAY
OUT. Wakaanza kutubu
dhambi zao. Mume akaanza
"Mke wangu kabla ya sijafa naomba unisamehe sana
kwani nilikuwa natembea na
mdogo wako na ile mimba
aliyotoa ilikuwa yangu".
Nisamehe mke wangu ili
Mungu nae anisamehe, huku akiwa amepiga magoti
Mke nae "sawa
nimekusamege. Ila na we
naomba unisamehe kabla
sijafa. Mume "sema tu mke
wangu nitakusamehe mbona we umenisamehe"........Mke
"Huyu mtoto wa mwisho sio
wako ni wa yule rafiki yako
kipenzi(pia ni jirani yao)
nisamehe mme wangu. Mme
akasikitika sana..... Mara anaingia mtoto yule yule wa
mwisho na kusema "Baba
yule mtu aliyemgonga mbwa
kwa baskeli kasema atakuja
kesho muongee. Ila mbwa
amepona nilikua nacheza nae sasa hivi kumbe alizimia
tu..VIPI KUHUSU HII NDOA
ITAENDELEA KWELI?