Daladala za Dar kama kawaida kujazana ndani ile ile, SASA kuna jamaa mmoja alikuwa na sh. 500 mfukoni mwake aliamua apande daladala hivyo hivyo alipoingia ndani akuweza hata kugeuka maana watu wamejaa ile mbaya........Basi konda alipoanza kuomba nauli ,Jamaa aliingiza mkono mfukoni na kutoa sh 10,000, jamaa kuona vile alimshukuru Mungu maana hakuwa na ile pesa, alipompa Konda alimrudishia Change na alishukuru tena na kuirudisha mfukoni tena...Basi aliamua kushukia kituo tofauti na kile ambacho anaenda, baada ya kushuka kuangalia mfukoni akajikuta na Ile sh. 500, Kumbe alipompa konda ile sh 10,000 aliitoa kwenye mfuko wa mtu, na aliporudishiwa change, aliirudisha kwenye mfuko wa mtu tena.